Latest Post

SHIDA SIO KULEA MIMBA SHIDA NI KULEA MTOTO

Written By zeenat singh on 26.11.16 | 26.11.16

Kuzaa sio kazi sana unaweza ukavumilia ukavuka sasa akitoka mtoto kulea mpaka awe ana akili na mtoto mwema hapo ndio kazi lazima mzazi ama mlezi uweke akili yako vizuri kulea mtoto sio kujaribu bali nia kulea akue.

NJIA GANI NZURI YA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO

Written By zeenat singh on 16.11.16 | 16.11.16

uzazi wa mpango ni jambo muhimu sana katika jamii yetu, lakini kuna njia nyingi sana ukitaka kupanga uzazi na familia nyingi waliotumia uzazi wa mpango wanasema hawajutii kutumia njia hizo....

lakini najiuliza ni njia gani nzuri ya kutumia? kwasababu watu wengine hupendelea kuweka vijiti japo wengine husema vijiti hivyo hutembea mwilini na kuleta madhara ya cancer.

wengine hutumia kitanzi, hiki hukaa muda mrefu wa miaka kumi lakini pia wengine huniambia tatizo la kitanzi style yako kamwe ni kifo cha mende maana ukijifanya unatoa machejo kinafyatuka, na wengine wanasema mwenza wako akiingia kinamtia kero kwa kumgasi...

na wengine wanatumia vidonge, lakini wengine husema ukikosea kumeza kimoja tu na ukacheza basi goli lazima liwe lako, na wengine wamepata ujauzito pindi wanatumia hizi dawa...

ama kutumia condom? sawa kwa mwanzoni mnaweza kutumia condom lakini mpaka lini, maana wanaume wengi wanasema yani mke wangu mwenyewe nimvalie condom???????????? ama kwa wale walevi najua pindi pombe zimekolea nivigumu sana kukumbuka condom....

je wewe umeshawahi kutumia njia za uzazi na ni ipi na je kunamadhara gani uliyokutana nayo???? maana kunawanawake wanaotaka kutumia njia hizi lakini hawajui ipi ni salama maana maneno yanasemwa mengi...

MWANAMKE UKIWA MLEVI LAZIMA USO WAKO UONEKANE MZEE

Written By zeenat singh on 14.11.16 | 14.11.16


Mwanamke kiukweli pombe haimpendezi kabisa maana kwa majukumu kama wanawake kwenye miji yetu ukipiga na pombe lazima msichana uonekane mtu mzima,na ndio inasababisha wasichana walevi ata kupata wanaume wa kuwaoa kazi maana mnaonekana wazee kumbe mkitulia na kunywa maji mengi ata ukiwa una umri mkubwa utaonekanabado unadai maana uuchoshi mwili wako na pombe.

WEMA NA CALISAHYani naumia sana nikiona mwanamke mtanzania na mwenye nyota na kupendwa kama Wema akitoka kwenye mitandao na kudhalilishwa hivi na uzuri nwake alionao sijui kabisa na sipendi namtetea Wema maana ni mwanamke mwenzangu atukatazwi kupenda ila tusiweke adharani na kama hii video katuma Wema umekosea sana lakini kama katuma mwanaume basi umemdhalilisha huyu mwana dada.Wema ukitulia ungekua mbali mno sielewi kua unashauriwa ya maana na ndugu zako na Mama uyafati ama vipi lazima ifike wakati ubadilishe mwenendo wa maisha yako kweli tena.

DAGAA NA MIHOGO NA KACHUMBALI YAM YAM

Vyakula vyetu vya asili ni vitamu na vina nguvu na kinga kwenye miili yetu kuliko hivyo vya kisasa  umeona utam huo bila shaka mate yamekujaa.

WIVU UKIZIDI KWENYE MAPENZI NI MBAYA SANA

Kweli tunasema wivu ni suna na ndio mwenza wako anajua unampenda,sikatai kabisa lakini jaribu kujua wivu wako unauweka sehemu gani na kwa wakati gani maana matokeo yake utakosa kabisa mapenzi kwa upendae sababu ya wivu wako matokeo yake mtaachana na utabaki unashangaa.

Lady Jaydee - NdiNdiNdi (Official Music Video) Lady Jaydee


wanawake Tunaweza ltd

 
Copyright © 2011. WANAWAKETUNAWEZA.COM - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger